Wednesday , 27th Sep , 2023

Uongozi wa klabu ya  Simba umesema wapinzani wao klabu ya Power Dynamos wanataraji kuwasili nchini Alhamisi ya kesho Septemba 27, 2023 kwa ajili ya mchezo wa marudiano CAFCL utaopigwa Oktoba Mosi uwanja wa Azam Complex Chamazi majira ya saa kumi jioni.

Akizungumza na Wanahabari, Meneja Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmedy Ally amesema wanatambua utakuwa ni mchezo ni mgumu dhidi ya Power Dynamos, hivyo wanakuja  Tanzania, sehemu ambayo hakuna aliyetoka salama.

“Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui."- Ahmed Ally. - Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC

Vile vile Ahmedy amesema  Mechi yao dhidi Dyamos ya Zambia  wataitumia kama maandalizi ya kuuendea mchezo wa Ufunguzi wa mashindano African Football League dhidi ya Al Ahly yanayotaraji kuanza  kutimua vumbi Oktoba 20, 2023 katika uwanja wa Benjamin MKapa, jijini Dar es salaam.

Simba SC inahitaji kupata ushindi wowote, suluhu ama sare ya bao 1-1 ili kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa mwaka 2023-24.