Monday , 25th Sep , 2023

Nahodha wa Newcastle United Kieran Trippier ndio mchezaji aliyekusanya alama nyingi zaidi kuliko mchezaji yoyote, kwenye Fantasy League katika michezo ya raundi ya 6 ya ligi kuu England EPL. Nafasi ya pili yupo Mitoma wa Brighton na James Tarkowski wa Everton ni wa tatu.

Trippier ameongoza wiki ya 6 baada ya kukusanya alama 18, Trippier ameisaidia timu yake ya Newcastle kuibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Shiffield United ambapo kwenye mchezo huo beki huyo wa upande wa kulia alitoa pasi 3 za magoli yani (assist). Kaoru Mitoma ametengeneza alama 14 baada ya kufunga mabao 2 kwenye mchezo dhidi ya AFC Bournemouth ambao Brighton ilishinda 3-1.

Nafasi ya 3 ni beki wa Everton James Tarkowski amekusanya alama 14 baada ya kuisaidia Everton kupata ushindi wake wa kwanza wa msimu dhidi ya Brenford wa mabao 3-1. Kwenye mchezo huo beki huyo wa kati alifunga bao 1 na alitoa pasi 1 ya goli (Assists).

Endelea kucheza na jiunge sasa na EA Radio Fantasy ili uibuke kuwa mshindi wa Shilingi Laki nne na nusu (450,000) kwa kuwa bingwa mshindi wa pili anashinda Laki moja (100,000) na mshindi wa tatu anaondoka na Elfu Hamsini (50,000). Jiunge sasa na EA Radio Fantasy league kwa kutembelea tovuti ya ww.fantasy.premierleague.com