
Mahakama ya rufaa ya uchaguzi iliamua katika uamuzi wa pamoja mapema mwezi huu kwamba Peter Obi wa chama cha Labour na Atiku Abubakar wa chama cha Peoples Democratic Party walishindwa kuthibitisha kuwa uchaguzi huo ulikuwa na dosari.
Mahakama hiyo ilitangaza kuwa wanasiasa hao hawakuweza kubaini madai ya wizi wa kura na ukandamizaji wa wapiga kura. Majaji pia walisema hakuna ushahidi wa kutosha kuunga mkono kesi hizo.
Bw Abubakar anaiomba mahakama ya juu kubatilisha uamuzi huo akisema kuwa ulileta "makosa makubwa na ukiukaji wa haki" kwa kuunga mkono ushindi wa Bw Tinubu.
Kupitia wakili wake, Bw Atiku pia alilaumu matumizi ya mahakama kwa "maneno ya kudhalilisha" ambayo alisema "yalithibitisha upendeleo".
Hakuna tarehe iliyowekwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi hizo.