Greenwood anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Getafe akitokea Manchester United, aliingia dakika ya 77 ya mchezo huo waliopata ushindi wa magoli 3 kwa 2 dhidi ya Osasuna, na ndio mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo.
Klabu ya Osasuna watakabiliwa na adhabu kutoka bodi ya ligi kuu Hispania La Liga baada ya mashabiki kumzomea na kumdhihaki Mason Greenwood katika mchezo dhidi ya Getafe, wakiimba "Greenwood, die"