
Wakazi wa eneo hilo wanasema wakati wa kiangazi hushuhudia foleni kubwa ambapo adha hiyo husababisha kukwama katika shughuli zao za kiuchumi kutokana na kusubiri muda mrefu.
Bomba hili lipo katika kijiji cha Oltushula ambapo wakazi kutoka vijiji vinne vya Oltushula, Lekamba, Nemburu na Oljorousu kutoka katika Musa hutegemea kuja kuchota maji wakilazimika kutembea umbali mrefu wakati mwingine kutumia Wanyama kama punda.
Mwenyekiti wa kijiji cha Oltushula Emmanuel Memute amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambapo amebainisha jitihada wanazoendelea kuzifanya ni pamoja na kuisisitiza mamlaka kuongeza miradi ya maji ili kukidhi mahitajikutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu.