Wednesday , 30th Aug , 2023

Mfanyabiashara wa madini Marwa Masese Festo (55) pamoja na mtoto wake John Marwa (30) wakazi wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, wameuawa baada ya kupigwa na vitu vizito kichwani na mmoja kufumuliwa ubongo na watu ambao ni marafiki zao maeneo ya Kata ya Wino, Halmashauri ya Madaba.

Gari la marehemu

Tukio hilo limetokea jana Agosti 29, 2023, ambapo baada ya marafiki hao kuwaua wakaweka miili ya marehemu hao kwenye gari lao aina ya Jeep grand nyekundu yenye namba T 241 DSX na kisha kwenda kulisukuma kwenye mteremko mkali ili ionekana kwamba wamefariki kwa ajali ya gari.

Imeelezwa kwamba watu waliotekeleza unyama huo ni watu wao wa karibu na marehemu hao na kwamba mmoja wa watuhumiwa hao ndio aliyewezesha marehemu Marwa kupata mwekezaji wa kuchimba madini katika kitalu chake kilichopo maeneo ya Amani Makolo wilayani Mbinga

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, amewaomba ndugu wa Marwa Masese Festo, kufika Songea kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao hao, na kwamba hadi sasa hivi watuhumiwa wawili wa tukio hilo wanashikiliwa na wote wamekiri kuhusika kwenye tukio hilo la mauaji.