Nyoni ametoa rai hiyo kwa vijana na wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kupata elimu juu ya mchezo wa Kabaddi huku akiamini wakufunzi hao wataongeza chachu ya maendeleo ya mchezo wa Kabaddi hapa nchini.
''Huu ni ugeni mzito katika nchini yetu hivyo kukaa kwao mwaka moja naamini kama sisi viongozi tutapata maarifa mengine kutoka kwao ''amesema Abdallah Nyoni.
Wakufunzi hao wawili wa mchezo wa Kabbadi wamewasili hapa nchini mnamo Agosti 26-2023 kwa ufadhili wa Serikali ya India pamoja na Serikali ya Tanzania kupitia Baraza La Michezo la Taifa (BMT) huku makocha hao wanataraji kukaa nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja.