Saturday , 12th Aug , 2023

Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia Said Mfaume (32) kwa kumchoma na kumjeruhi mpenzi wake katika maeneo mbalimbali ya mwili wake kisha na yeye kujaribu kujiua.

Kamanda wa Polisi Mwanza Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea tarehe 6 Agosti, 2023 katika nyumba ya kulala wageni baada ya kuzuka ugomvi baina yao uliotokea baada ya binti huyo kukataa kuolewa na mtuhumiwa.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa ameshatoa mahari kwa mama wa binti huyo bila binti huyo kuridhia kuolewa naye hivyo baada ya kukutana na binti huyo na kujaribu kumweleza mipango ya ndoa akakataa ndipo akaamua kumjeruhi kwa kisu kisha naye kujichoma maeneo ya tumbo #EastAfricaRadio