Monday , 7th Aug , 2023

Simba wawili waliozua taharuki maeneo mbalimbali ya vijiji vya mikoa ya Njombe na Iringa, hii leo Agosti 7, 2023, wameuawa katika kitongoji cha Lole, Kijiji cha Makungu wilaya ya Mufindi kwa ushirikiano wa Askari wa Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Kipengere

Simba waliouawa

Mkuu wa Hifadhi ya Kipengere mkoani Njombe, Donasiani Makoye, amesema Simba hao walitoweka Hifadhini Julai 21 mwaka huu na wao waliendelea kuwafuatilia Simba hao na leo wamefanikiwa kuwaua 

Mhifadhi huyo amekiri kuwa Simba hao wamesababisha madhara makubwa kwa kushambulia na kuua ng'ombe 14 na nguruwe 5.

Aidha Mhifadhi huyo Amesema wao Kama Jeshi la Uhifadhi wanaendelea kuchukua hatua zaidi ili kuwadhibiti Simba hao ikiwa pamoja na kuwafungia mfumo wa mawasiliano ya utambuzi 

Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Makungu wamesema kwa muda mrefu wameshindwa kuendelea na majukumu yao kwa kuhofia Simba hao. 

Wananchi  wamesema wanawashukuru Askari hao wa Hifadhi ya Kipengere