Sunday , 6th Aug , 2023

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa ametoa onyo kwa watu wanaojipanga kufanya uhalifu katika maonesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongoro jijini humo

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa baadhi ya mabanda eneo hilo amesema wananchi wawe na amani kuendelea kujitokeza kutembelea na kujifunza katika mabanda mbalimbali taliyopo katika maonyesho hayo

Ameongeza kuwa katika kuweka elimu usalama na namna ya kujikinga dhidi ya wahalifu, jeshi hilo limeweka banda lake ambalo linatoa elimu hiyo na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza

Aidha amesema hali ya usalama katika uwanja huo ipo shwari na watu wanaendelea kuadhimisha kwa amani.