Saturday , 5th Aug , 2023

Mkazi wa Kijiji cha Zambia wilayani Kiteto mkoani Manyara, Issa Juma Rashidi (25) amekutwa dukani kwa mama yake akiwa amefariki huku shingo yake ikiwa imekatwa na kitu chenye ncha kali.

Wananchi wakiwa nje ya duka

Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ramadhani Hassani Yusuph amethibitisha tukio hilo na kusema mapema asubuhi ya leo Agosti 5, 2023,  amepata taarifa hizo na kufika eneo la tukio na kujulisha Jeshi la Polisi Kituo kidogo cha Kijungu na kufika hivyo uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.