Tuesday , 1st Aug , 2023

Uongozi wa Yanga Sc umesema umeshawasilisha majina ya wachezaji wote waliowasajili kwa ajili ya kutumika katika msimu ujao 2023 -2024 kwa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF kwa ajili ya kuwaingiza katika mfumo wa usajili.

Taarifa hiyo imetolewa na Afisa habari wa Yanga  SC Ally Kamwe kuwa majina yote ambayo benchi la ufundi waliwasilisha  katika ofisi ya mtendaji wa Yanga SC yameshapelekwa hivyo mashabiki wasiwe na presha kwani kila mchezaji waliyemuona hatatumika katika mashindano.

“Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri hatuna majeraha hadi muda huu hivyo tunasubiri kwenda mkoani Tanga kwenda kuchukua kombe letu “amesema Ally Kamwe.

wakati huo huo Kamwe ametoa pongeza kwa klabu zote zinazoshiriki Ligi kuu NBC Tanzania msimu ujao  kwa kufanya usajili mzuri na wenyewe kutoa ushindani katika Ligi yetu .