Thursday , 20th Jul , 2023

Jina lake kamili ni Raila Amolo Odinga lakini wengi nchini Kenya humuita Baba,Jackom,Arap Mibei na Rais wa wananchi.

Alizaliwa mnamo mwaka 1945 katika kaunti ya Kisumu eneo la masemo nchini Kenya akiwa ni mtoto wa Makamu wa kwanza wa Rais wa Kenya Jaramongi Oginga Odinga chini ya Rais wa kwanza wan chi hiyo Jomo Kenyata.

Odinga anajulikana kama moja ya wanasiasa wakonge na mashuhuli akihudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo waziri mkuu wa Kenya kutoka mwaka 2008 hadi mwaka 2013,pia amekuwa Mbunge wa langata kuanzia mwaka 1992 hadi mwaka 2013 na nafasi mbalimbali za uwaziri katika serikali ya Kenya.

Pia Odinga anatambulika kama kiongozi mkuu wa upinzani nchini Kenya kupitia umoja wa vyama vya upinzani nchini humo ukijulikana kama Azimio la umoja,pia amewahi kuwa kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement ODM.

Kwa takribani mara tano kiongozi huyu mkuu wa upinzani aligombea nafasi ya Urais lakini mar azote hakufanikiwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo na kuweza kuliongoza taifa la Kenya licha ya Katiba ya nchi hiyo kuruhusu matokeo ya Urais kupingwa Mahakamni lakini bado alshindwa kufua dafu na kubakia kuwa mgombea aliyewahi kushiriki kama wagombea wengine.

Mwaka 1997 Odinga alimaliza nafasi ya tatu kama mgombea wa Urais kupitia tiketi ya chama cha National Development Party (NDP),Mwaka 2007 aligombea nafasi hiyo hiyo kupitia chama cha Orange Democratic Movement (ODM)akichuana na Mwai Kibaki lakini alipoteza na Kibaki kuwa Rais.

Odinga hakukata tamaa, bado aliendelea kujipa tumaini na kuamini kuwa nafasi ya kuwa Rais wa Kenya bado ipo,Jambo  hili  likampa nguvu yakugombea tena mwaka 2013 kupitia chama cha Coalition for Reforms and Demokracy(CORD) na mwaka 2017 akigombea kupitia chama cha National Super Alliance (NASA) na kivumbi na jasho ilikuwa mwaka  2022 dhidi ya Rais aliyeko madarakani kwa sasa William Ruto akiwa na Muungano wa Azimio la Umoja  na bado alipoteza tena nafasi  hiyo na kisha kwenda mahakamani kufungua kesi ambayo  ilikuwa na mvuto mkubwa  wa kisiasa na kuvuta hisia za watu wengi katika nchi za Afrika Mashariki na kwa bahati mbaya alishindwa kesi hiyo.

Kwa sasa Odinga anashuhudiwa kuitisha maandamno makubwa ya wananchi  kupitia Muungano wa Azimio huku sababu  kuu ambayo aliitoa katika hotuba yake mapema mwezi February mwaka huu akiitisha maandamno hayo kwa mara ya kwanza alisema ni kupanda kwa gharama za maisha .

Tangu kumalizika kwa maandano ya wiki iliyopita kwa wiki hii yote Raila Amolo Odinga hajulikani alipo na hata maandamano yaliyofanyika wiki hii Odinga hajaonekana hadharani wala kwenye vyombo vya habari na hakuna taarifa yoyote ambayo inaeleza Odinga yupo wapi.