Thursday , 20th Jul , 2023

Kenya imeingia katika siku ya pili ya maandamano hii leo, ambapo kumeripotiwa hali ya utulivu wa jumla na shughuli ndogo nchini humo siku ya Alhamisi asubuhi

Barabara nyingi katika miji mikubwa zimebaki zimetengwa na biashara bado zimefungwa.

Katika shule ya msingi ya Moi Avenue, shule iliyoko jijini Nairobi, wazazi waliripotiwa kuogopa kuwapeleka watoto wao shuleni na wanafunzi wachache tu ndio walioripoti.

Hali kadhalika ilishuhudiwa katika Kaunti ya Kisumu ambapo shule kadhaa za siku zilisalia kufungwa.

Waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki na mwenzake wa elimu Ezekiel Machogu waliagiza shule zote kufunguliwa tena Alhamisi akisema usalama umetathminiwa katika miji mitatu mikubwa.

Katika mji wa Homa Bay, sehemu ya vijana walifunga barabara kwa mawe kabla ya maandamano.

Polisi  wamelaumiwa na wapinzani nchini humo kwa kutumia nguvu, ambapo wamesema polisi wamempiga kijana mmoja risasi licha ya kwamba kijana huyo hakua kwenye maandamano.