
Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse, akipata maelekezo
Moja ya wadau hao ni Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse ambaye Jumanne tarehe 4 Julai 2023 ametembelea banda la GGML katika maonesho hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Dk. Mwasse alipata maelezo kutoka kwa Afisa Manunuzi (Mikataba) wa GGML, Silas Shija (wa kwanza kulia) aliyekuwa ameambatana na Scholastica Hoya, Ofisa Rasilimali Watu na Innocent Mushi ambaye ni Ofisa Mwandamizi (Rasilimali Watu).
Walieleza jinsi GGML inavyosaidia miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika jamii zinazozunguka migodi yake kama vile elimu, afya, maji, miundombinu na kilimo.
Miradi hii inaakisi dhamira ya GGML kwa jamii inayozunguka mgodi kuwa na maendeleo endelevu.
Mojawapo ya maadili yake ya msingi, na maono yake ni kutoa mchango chanya.