
na kupitishwa na Bunge kwa kutengeneza sheria zitakazotumika kuongoza mikataba ya Ubinafsishaji wa bandari kwa kampuni ya DP World ya Dubai hadi Julai 20 mwaka huu
Kesi hiyo ambayo imepangwa kusikiliwa na majaji wa tatu ilikuwa inasikiliwa na jaji Dustani Nduguru ambapo Wajibu Maombi (Wakili Serikali) waliomba mahakama isogeze mbele ili kupata fursa ya kukusanya vielezo vya waleta maombi baada ya mvutano wa mda mrefu Mahakama amewaaigiza wajibu na waleta maombi kuwasilisha nyaraka Julai 14 ili kesi ianze kusikilizwa mfululizo kuanzia Julai 20
Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama kuu kanda ya Mbeya na Emmanuel Kalikenya Chengula, Alphonce Lusako, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi wakimshtaki mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Uchukuzi,katibu wa Wizara ya Uchukuzi na katibu wa Bunge
Kesi hiyo inasimamiwa na mawikili wa kujitegemea Bonface Mwabukusi, Philip Mwakilima, Livino Haule na Caroline Luhungu.
Mawakili wa Serikali ni Hangi chanya Wakili wa serikali Ayoub Sanga wakili wa Serikali (SA)
Kesi hiyo inasikiliwa na majaji watatu wa Mahakama kuu
Majaji wengine walipongiwa kusikiliza kesi ya kikatiba ni Abdi S Kagomba (mahakama Kuu Dodoma
Akizungumza nje ya Mahakama mmoja wawalamikaje Alphonce Lusako asema amesema sababu ya kugungua kesi hiyo ni kutaka kupata tafsiri kisheria na kwamba hawapinga suala la uwekezaji lakini wanapinga baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye mkataba huo.