Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba, na kulia ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Ndugu Chongolo amesema hayo leo Juni 18, 2023 baada ya kukagua mradi wa Umoja wa Wakulima wa Zabibu wa ICHIMADA ulioko eneo la Chinagali, pamoja na Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa ‘Jenga Kesho Iliyo Bora' (BBT) uliopo katika eneo hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Chongolo amesema kuwa dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,ni kuona miradi ya kilimo inaleta tija kwa haraka, hivyo ni muhimu miradi hiyo isiwe na majina mazuri tu, bali ilete matokeo na manufaa kwa wananchi.