Tuesday , 13th Jun , 2023

Rayson Agnelusi Duwe ambaye ni muuguzi  msaidizi daraja II (ANO)  katika hospitali ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumbaka mama mgojwa mwenye ujauzito wa miezi tisa  baada ya kumchoma sindano yenye dawa ya usingizi

Kamanda wa Jeshi la polisi  mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao  amesema tukio hilo lilitokea Juni 9. 2023  majira saa mbili usiku

Kamanda Abwao amesema  muuguzi huyo ambaye aliingia kazini akiwa amelewa pombe  alitenda  kosa hilo wakati alipopangiwa  zamu ya usiku  ya kuhudumu wagonjwa wa nje  (OPD)  ndipo alipotoka  na kwenda  chumba cha wagonjwa wa ndani na  kumbaka mama huyo mwenye ujauzito wa karibu kujifungua ambaye  alikuwa anaendelea na matibabu ya ugojwa wa malaria.

Muuguzi huyo alikutwa akiwa na bomba  la sindano  pamoja na dawa za usingizi  huku taarifa ya kitabibu ikidhibitisha  kuwa alimwingilia mgonjwa huyo.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakani mapema hii leo June 13,2023 kujibu tuhuma zinazomkabili  baada  ya upelelezi kukamilika