Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa
Kauli hiyo ameitoa bungeni hii leo Juni 2, 2023, wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, "Shirika litajenga studio ya kurusha vivutio vya utalii mubashara utakaowezesha vivutio kurushwa moja kwa moja kwenye mitandao na chaneli za kimataifa,"
Aidha amesema kwamba kuongeza kuwa kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini kumevunja rekodi ya mapato katika Hifadhi za Taifa Tanzania.
"Taasisi za utalii nchini zimevunja rekodi ya mapato katika maeneo yao, mfano TANAPA kwa mwaka mzima wa 2021/22 walikusanya TZS bilioni 174, kwa miezi 10 tu ya mwaka huu wa fedha, wameshakusanya TZS bilioni 291 mapato haya kwa taasisi ni makubwa kuliko yoyote yaliyowahi kukusanywa tangu zianzishwe," amesema Mchengerwa
Aidha, mapato haya yametokana na juhudi zilizofanyika za pamoja kutangaza vivutio vya utalii na kuimarika kwa miundombinu ya utalii ndani ya hifadhi.
Wizara ya Maliasili na Utalii leo imewasilisha makadirio ya Bajeti ya jumla ya shilingi 654,668,208,000 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 matumizi ya fungu 69 kwa mwaka wa fedha. Kati ya fedha hizo TZS 486,501,449,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na TZS 168,166,759,000 ni za miradi ya maendeleo.