Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Akiwa kwenye ziara mkoani Iringa wananchi wa kijiji hicho waliangua kilio mbele ya Katibu Mkuu wa CCM baada ya mradi wa maji kusuasua licha ya mkandarasi anayejenga mradi huo kulipwa.
Aweso amekiri kuwa kuna uzembe ulifanyika kwenye utekelezaji wa mradi huo na kwamba ndio sababu ya kukwama na akaahidi kuukamilisha ndani ya miezi mitatu ili tatizo la uhaba wa maji kwenye eneo hilo liishe.
Amewataka watendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) pamoja na viongozi wa Mkoa wa Iringa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kila wiki.
Katika hatua nyingine,Aweso amewaomba wananchi wa eneo hilo kuwa wavumilivu wakati Wizara yake inaendelea kukamilisha mradi huo.