Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la serikali ya Uturuki, Anadolu, mfungamano wa vyama unaoongozwa na rais Erdogan ulipata asilimia 49.39 ya kura wakati mfungamano wa vyama vya sita vya upinzani unaoongozwa na Kemal Kilicdaroglu ulifikia asislimia 44.92.
Hadi sasa zaidi ya asilimia 90 ya kura zote zilizopigwa zimeshahesabiwa. Duru ya pili ya uchaguzi huenda ikafanyika tarehe 28 mwezi huu. Rais Erdogan mwenye umri wa miaka 69 amekuwamo madarakani kwa miaka 20.
Matokeo, kamili yatajulikana baada ya duru ya pili ya upigaji kura iwapo itaamriwa hivyo na tume ya uchaguzi, ndio yataamua kama nchi ya Uturuki, mshirika huyo wa jumuiya ya NATO kama bado itatawaliwa na Erdogan au utawala wa nchi hiyo utachukuliwa na mpinzani wake mkuu Kemal Kilicdaroglu.