Eddy Kenzo
Eddy anayefanya poa na ngoma yake ya Sitya Loss katika chati mbalimbali ameweka wazi kuwa, miongoni mwa ngoma atakazoachia itakuwepo Jambole aliyoshirikiana na Kcee na vilevile Royal aliyofanya na Patorankin, vilevile Number Yo na Mariaroza.
Hii inakuwa ni zawadi kubwa kabisa kwa mashabiki wa star huyo ambaye amesema ana uhakika kuwa mzigo huo utakubalika na watu kutokana na ladha na mitindo tofauti ambayo imetumika ndani yake.