Friday , 14th Apr , 2023

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kwamba kwa mujibu wa sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria ya Tanzania, imetamka bayana kwamba vitendo vya mapenzi ya jinsia moja au kinyume na maumbile iwe kwa faragha au kwa makubaliano ni kosa la jinai.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 14, 2023, bungeni jijini Dodoma wakati akitoa tamko kufuatia hoja iliyojadiliwa bungeni humo kuhusu vitendo vya mmomonyoko wa maadili na vitendo vinavyokwenda kinyume na mila, tamaduni na desturi za Mtanzania.

"Sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria ya Tanzania inatamka bayana kwamba vitendo vya mapenzi ya jinsia moja au kinyume na maumbile iwe kwa faragha au kwa makubaliano ni kosa la jinai," amesema Waziri Mkuu 

Waziri Mkuu amesema kwamba uwepo wa matukio na vitendo hivyo umekuwa ukihatarisha uimara na ustawi wa familia na Taifa kwa ujumla.

Tazama video hapa chini.