Wednesday , 9th Nov , 2022

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imebainisha kuwa maelfu ya namba za simu zilizojihusisha na wizi, utapeli na ulaghai kupitia Mtandao wa simu zimefungwa

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt Jabiri Bakari, amesema jumla ya namba tambulishi 52,087 zikiwemo zilizoripotiwa kupotea, kuibiwa au kuhusika katika matukio ya kihalifu zimezuiliwa kupokea na kutoa huduma za Mawasiliano.  

Amesema Kuanzia Julai 2021 hadi kufikia Septemba 2022 jumla ya namba tambulishi zilizofungiwa na mfumo huu ni 52,087 ambazo ziliripotiwa kupotea, kuibiwa au kuhusika katika matukio ya kihalifu, hivyo kuwezesha kupunguza matukio ya wizi na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya Mawasiliano vyenye ubora kwenye soko.