Monday , 10th Oct , 2022

Biashara ya mirungi Mkoa wa Kilimanjaro imekithiri, huku ikisafirishwa mchana waziwazi kwa pikipiki hali hiyo imetajwa kuleta taharuki miongoni wa wananchi wakiziomba mamlaka kufanya operesheni kabambe.

Baadhi ya wasafirishaji wakubwa wa mihadarati hiyo wameunda magenge ya kihalifu ambayo hujihami kwa mapanga na hutumia pikipiki kusafirisha mirungi kwa mwendo wa kasi kutoka mpaka wa Kenya hadi katikati ya mji wa Moshi.

Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya askari polisi wasio waaminifu wanaokuwa kwenye magari ya doria na wale wa kitengo cha Intelijensia, wanadaiwa kuonekana wakiwakamata wahalifu lakini ndani ya muda mfupi huachiwa.

Mirungi hiyo ambayo ni biashara inayowapa utajiri baadhi ya wafanyabiashara, imekuwa ikiingizwa nchini kutoka Kenya kupitia maeneo ya Kitobo, Madarasani, Tarakea na Mnoa na kusafirisha hadi Moshi, Arusha na Babati na mikoa mingine.