
Wakizungumza na EATV mkoani humo baadhi ya wananchi wanasema wamekuwa wakipunjwa kwenye bidhaa wanazonunua huku wakiwa hawana elimu na wapi kwa kuwashtaki wafanyabiashara wanaofanya vitendo hivyo.
"Kwakweli tunapunjwa kilo ya sukari imepunguzwa kilo la mchele imepunguzwa mizani yake Sasa mimi nachoongelea kuhusu serikali iweze kukineba hili ilione kama pana uwezekano wa kuwa wanawachunguza baada ya mwezi wanakuja wanazipima zile mizani zao wanazichunguza kama zipo salama mimi naona hilo litakuwa bora zaidi kuliko kuziangalia tu au kuwaangalia tu mradi wanalipa kodi sijui wanalipa nini hiyo custom duty hapana wawe wanakuja kuchunguza zile mizani zao mara kwa mara", alisema Daudi.
"Tunawaomba hawa watu wa vipimo wawe wanapita wanatupa semina kwamba wanapunja vipi na kila sekta kiukweli, na kila sekta ina ujanja wake jinsi ya kufanya nini, jinsi ya kupata hela inamaana kwa njia ya wizi yani ni kama kiini macho kuna vitu anatengeneza anairekebisha Ile scale kwahiyo kama ni gram moja na nusu wewe inasoma gram inamaana wewe anakuibia nusu gram kwahiyo tunaomba kwamba wananchi tueleweshwe jinsi ya kwamba kutambua hii ni imeongezwa au hii ni halal tunaomba elimu hiyo", alisema Mwangosi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa huduma za biashara wakaka wa vipimo Deogratius Maneno amewataka wananchi kuangalia alama zilizo kwenye mizani ili kugundua kama mizani hiyo ipi sahihi ili kuepuka kupunjwa wanapohitaji kufanya manunuzi.
"Wakala wa vipimo kila tunapofanya uhakiki kuna alama maalum huwa tunaweka, kipimo hiki kimehakikiwa kwahiyo kunakuwa na sticker maalum inayowekwa kuonesha mzani huu au kipimo hiki au kituo cha mafuta kimekaguliwa mara ya mwisho lini na Ile sticker, pamoja na sticker ndani kunakuwa na seal ambayo hawezi kuikata yule akiikata maana yake wakala wa vipimo watagundua amefanya kosa kisheria kwahiyo tunawaalika kwa wale wote amabo mnafanya biashara, mnaoenda kununua na wale wauzaji hakikisha mzani wako kama ni kipimo kidogo kile cha madukani una sticker na wananuzi tunawashauri usiende kununua either mafuta au usiende kununua kwenye mzani ambao unaona hauna sticker", alisema Maneno.
Aidha Maneno anasema wameandaa semina kwa ajili ya wajasiriamali wadogo namna bora ya kufungasha biashara zao kwa kuzingatia vipimo ili waweze kupata faida inayoendana na vipimo.
"Tunafanya ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwa mengo la msingi ni kuona kwamba mtu ananunua anapata thamani ya fedha yake na mtaona hapa pana wajasiriamali wengi tumepata nafasi ya lwensa kuongea nao tumeshapata anuani zao hivi tunatarajia kwa maelekezo ya viongozi wetu kipindi kifupi kijacho tutafanya nao mafunzo maalum kwa ajili ya kuwapa elimu ya ufungashaji bora", alisema Maneno.