Saturday , 17th Sep , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amewasili London nchini Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Pichani anaonekana kizungumza na Muwakilishi wa Mfalme Charles III, Cynthia  Gresham  pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Luton tarehe 17 Septemba, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza takayofanyika tarehe 19 Septemba, 2022 Jijini London.