Wednesday , 31st Aug , 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Godwin Gondwe ameipongeza kampuni ya Simu ya Vodacom kwa kuwa ya kwanza kwenye kuleta mabadiliko yanayoigusa jamii moja kwa moja.

Akizungumza hapo jana Agosti 29,2022 alipotembelewa na washindi wa bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya ‘M Pesa imeitika’, Mheshimiwa Gondwe alitanabaisha kwamba Vodacom wamekuwa vinara katika mapinduzi ya teknolojia na huduma zinazonufaisha Watanzania wote.

“Vodacom imeweza kuwa ya kwanza kwa kufanya M PESA, Vodacom imeweza kuwa ya kwanza M PAWA, Vodacom imeweza kuwa ya kwanza M MAMA na M MAMA inasaidia kina mama kuweza kufika hospitalini haraka na wakapata huduma, ni jambo kubwa sana. Lakini pia Vodacom wameweza kuwa kwanza 4G kwa hiyo sisi kama Serikali tunawapongeza sana” amesena Mheshimiwa Gondwe.

Nao washindi wa zawadi za bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya M Pesa Imeitika, Magdalena Magoma na Beata Madachi, wameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yanayoziwezesha kampuni kama Vodacom kuweza kufanya kazi kwa faida nchini, jambo linalonufaisha vijana kama wao na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Mheshimiwa Godwin Gondwe alisema kupitia ‘M Pesa Imeitika’ na huduma nyingine za Vodacom, vijana wanafikiwa na kuweza kutengeneza ajira akitolea mfano kwamba bajaji na pikipiki zilizotolewa zitatoa ajira kwa vijana.

Kampuni ya Vodacom inaendelea kuwa kinara kwa kuwa wa kwanza katika mapinduzi ya kidigitali na kuwa na huduma zenye ubora na kugusa maisha ya Watanzania.