Monday , 29th Aug , 2022

Serikali imesema inajenga mfumo mpya wa Ununuzi baada ya changammoto kadhaa kuukumba mfumo wa Taneps unaotumika kwa sasa 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)

Imeelezwa kuwa serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeamua kuwatumia wataalamu wa ndani ili kujenga mfumo utakaoweza kutatua changamoto zote zilizokuwepo kwenye Mfumo wa zamani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi amesema changamoto mojawapo ilikuwa ni wafanyakazi kufanya kazi za Ununuzi hata kama hatambuliki na Bodi na alikuwa anaweza kufanya shughuli za Ununuzi bila kukidhi vigezo vilivyowekwa na Bodi 

Amesema hii ilikuwa inapelekea kuwepo kwa madhaifu mengi kwenye shughuli za Ununuzi na wakati wa ukaguzi wa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali alipokuwa anafanya ukaguzi wake alikuwa anakuita madhaifu mengi kwenye ununuzi wa umma.

Mbanyi amesema hata wale ambao sio wataalamu wa Ununuzi walikuwa na uwezo wa kutumia mfumo wa zamani lakini mfumo huu mpya mtaalamu yoyote hata kama ni afisa manunuzi mwandamizi au afisa manunuzi wa cheo chochote kama hana usajili wa Bodi ya PSPTB hatoweza kuingia kwenye Mfumo huo