Tuesday , 27th Jan , 2015

Kikosi cha timu ya Azam FC ya Tanzania kimeelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuweka kambi ya wiki moja.

Azam wataweka kambi hiyo katika kujiwinda na michuano ya kombe la klabu bigwa barani Afrika, ambapo kikosi cha wachezaji 24 watajumuika katika msafara huo na viongozi wao.

Kambi hiyo itachukua muda wa wiki moja wakiwa huko watacheza michezo ya kirafiki kwa kupambana na TP Mazembe, Don Bosco ya Kinshasa na Zesco ya Zambia.

Timu hiyo itarejea Jijini Dar es Salaam Februari 4, tayari kwa mchezo wa kwanza wa klabu bigwa Afrika dhidi ya EL Merreikh ya Sudan Februari 15, utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.