
Kamanda wa polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale
Kamanda wa polisi mkoani Kagera William Mwampaghale, amesema kuwa wizi huo ulifanyika Julai 12 mwaka huu, na kwamba baada ya polisi kupata taarifa waliweka mtego na kufanikiwa kuwapata katika Kijiji cha Mgera, Kata Nyantakala wilayani humo, wote wanne wakiwa wamepanda pikipiki moja, na waliposimamishwa wakakaidi, polisi wakafyatua risasi na kuwajeruhi watu wawili.
"Mtu mmoja ambaye hajafahamika jina alifariki wakati anapelekwa hospitalini, huku wengine watatu akiwamo mmoja aliyejeruhiwa kwa risasi walifanikiwa kutoroka na tunaendelea kuwatafuta, katika eneo la tukio kulipatikana pikipiki iliyotumiwa na wahalifu hao yenye namba za usajili MC 489 DJH, fedha noti za shilingi 355,000 na sarafu shilingi 22,250" amesema RPC Kagera Mwampaghale