Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, imekubaliana na maagizo nane ya bunge kuhusiana na sakata la akaunti ya fedha ya Tegeta Escrow na kuiagiza serikali kutekeleza maazimio ya bunge kama ilivyopendekezwa na kuwataka walewote waliopewa dhamana ya uongozi kuwajibika katika nyazifa zao kwa kuzingatia maadili.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameelezea maazimio ya kikao hicho kilichoketi mjini Zanzibar na kuongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Rasi Jakaya Kikwete.
Kuhusu adhabu iliyokuwa imewekwa na chama hicho kwa waliotangaza nia ya kugombea nafasi ya uraisi katika
uchaguzi wa mwaka 2015, Nape amesema kuwa kamati imeiagiza kamati ndogo ya maadili kuketi tarehe 19
January ili kutathmini adhabu hiyo na utekelezaji wake na kuleta maazimio ya kamati ndogo ya maadili kwa
kamati kuu itakayoketi mwezi February kuyapitia.
Aidha sakata la ununuzi wa mahindi toka kwa wakulima kamati imeiagiza serikali kupitia upya mfumo wa ununuzi
wa mahindi toka kwa wakulima ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata stahiki zao,.
Kikao hicho cha kawaida kilichoketi mjini Zanzibar kikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, kilichodumu kwa masaa nane na kutoka na maazimio manne ikiwemo sakata la escrow, hali ya kisiasa na mambo mengine.
Watuhumiwa sita waliokuwa kwenye kifungo hicho cha chama cha mapinduzi ni Stephen Wassira, Wiliam Ngeleja, January Makamba, Fredrick Sumaye, Edward Lowassa na Bernad Membe.