
Ulrich Matei, Kamanda wa Jeshi la Polisi - Mbeya
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya ASP Ulrich Matei amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori la mizigo lenye namba ya usajili T 906 DQC.
Kamanda Matei amesema roli hilo lilifeli breki na kuparamia magari mengine katika mteremko wa Iwambi uliopo mjini Mbalizi, Mach 27, 2022 katika barabara ya Mbeya - Tunduma. Vyombo vingine vilivyohusika katika ajali hiyo ni Bajaj aina ya TVS, Toyota Nissan, Toyota Noah, Pikipiki aina ya T-Better. Wahanga wa ajali hiyo ni watu tisa huku kati yao watano walifikishwa hospitalini wakiwa tayari wameshapoteza maisha, na majerehi ni wanne.