Thursday , 8th Jan , 2015

Msanii na Mtayarishaji muziki kutoka Studio ya The Industry, Nahreel Mkono amezungumzia kilio cha muda mrefu cha watayarishaji muziki wengi hapa Tanzania, kupata kipato kidogo kutoka katika rekodi za muziki wanazozitengeneza.

Msanii wa bongofleva Nahreel Mkono

Nahreel amesema kuwa kiuhalisia huwapatia wasanii kipato kikubwa tofauti na kipindi cha nyuma.

Nahreel amesema kuwa, kiuhalisia Mtayarishaji muziki yeyote ambaye anajaribu kujikwamua kutoka hali hii na kupandisha bei ya huduma zake, husababisha wasanii kumkimbia na hivyo kuwalazimu kuendelea kuumia ili kuendelea kufanya kazi na wasanii hao.