
(Nembo ta TFF pamoja na mashabiki wa Yanga SC na Simba SC 2022)
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo imekemea vikali wale wote wanaofanya vitendo hivyo na imeanza kukusanya ushahidi wa matukio yote ya aina hiyo kupitia kamera za kurekodi matukio (CCTV) zilizoko uwanjani.
Aidha TFF iliwataka watu wote wanaohusika na vurugu kwenye Mpira wa Miguu (washabiki pamoja na viongozi) watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
TFF imeeleza kuwa wale wote wanaotoa shutuma kwa viongozi na maneno ya kuhamasisha vurugu katika Mpira wa Miguu nao watachukuliwa hatua hizo kwa mujibu wa kanuni zilizopo.
Kanuni kuu ya Mpira wa Miguu ni mchezo wa kiungwana (fair play) ndani na nje ya uwanja, hivyo wadau wote wa Mpira wa Miguu wajiepushe na vitendo vya vurugu ili kulinda heshima ya mchezo huo unaoongoza kwa kuwa na washabiki wengi Duniani.