Wednesday , 16th Feb , 2022

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi.Neema Msitha amewataka waamuzi kutunza ladha ya mpira wa miguu kwa kutumia taaluma na kufanya kazi kwa weledi ili kujitofautisha na wasiokuwa na taaluma hiyo.

(Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Taifa, Bi.Neema Msitha)

Aidha Msitha amewasisitiza ametoa wito kwa TFF kuona umuhimu wa kuwaleta wataalamu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa TAKUKURU wawe wanahudhuria katika Semina hizo ili waamuzi wapewe Elimu kuhusu rushwa.

Mwamuzi Heri Sasii amewashukuru TFF pamoja na bodi ya ligi kwa kuandaa kozi hiyo ambayo itaendelea kuwakumbusha na kuwaongezea ujuzi huku akiwaahidi watanzania wataendelea kuwa na weledi na kutenda haki.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Nassor Hamduni ameeleza kuwa semina hizo ni mwendelezo kozi za mara kwa mara ili kuwakumbusha waamuzi dhamana yao kwa jamii na wachezaji lakini pia kuendana na wakati kwakuwa kila siku mambo yanabadilika.