Saturday , 8th Jan , 2022

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho, amempongeza aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, kwa kitendo chake cha kiungwana cha kujiuzulu na kusema ndani ya uongozi ukiona umeteleza jiuzulu, kaa pembeni, jitafakari na urejee upya.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Odo Mwisho

Amesema kuwa kujiuzulu kwa Job Ndugai haimaanishi kwamba yeye sio kiongozi mzuri lakini hakuchagua maneno ya kusema na kwa wakati gani na akiwa nje atajitafakari na kujifunza.

Aidha, Mwisho amesema kuwa CCM haiwezi kugawanyika kwa sababu hakuna aliye mkubwa kuliko chama hicho, na kwamba bado kipo imara.