Saturday , 13th Dec , 2014

Msanii na mtayarishaji muziki Lovy Longomba Kutoka katika kundi la Longomba anatarajia kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki ambaye kazi yake imeingia katika tuzo za Grammy

Lovy Longomba

Msanii na mtayarishaji muziki Lovy Longomba Kutoka katika kundi la Longomba ambalo limeacha historia nzuri katika chati za muziki Afrika, anatarajia kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki ambaye kazi yake imeingia katika tuzo za Grammy ikiwa na matarajio ya kufanya vizuri na kunyakua tuzo mwanzoni mwa mwaka ujao.

Hii ni kutokana na ushiriki wake katika matayarisho na kuandika ngoma ya rapa Iggy Azalea inayofahamika kwa jina Change Your Life akishirikiana na Rapa TI, rekodi ambayo ipo ndani ya albam ya The New Classic ya mwanadada huyu ambayo ipo katika kipengele cha albam bora ya rap katika Grammys.

Lovy ambaye kwa sasa anaendesha shughuli zake za muziki huko Marekani, kwa njia ya mtandao ametoa shukrani zake kwa Mungu, Mashabiki na Familia yake kwa mafanikio haya makubwa kwa sanaa yake kimataifa.

Longombaz