Farouk Shikalo kushoto akiwa na Metacha Mnata
6. Ni idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa na klabu ya Geita Gold ya mkoani Geita ikiwa ni maandalizi ya ujezi wa kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania bara ambapo klabu hiyo itakuwa ikishiriki ligi kuu kwa mara ya Kwanza.
Wachezaji hao sita ni Salum Ayee, Often Chikola, Yusuph Kagoma, Idd Mfaume Mobby, Daniel Ruben Lyanga na Kelvin Nashion Naftali. Hawa ni wachezaji wapya lakini pia klabu hiyo imewapa mikataba mipya wachezaji 10 waliokuwa sehemu ya kikosi kilichoipandisha timu hiyo daraja kutoka daraja la kwanza mpaka ligi Kuu.
5. Ni miaka ya mkataba mpya anaotarajia kusaini beki wa kati wa timu ya taifa ya England John Stones na klabu yake ya Manchester City mkataba utakaomfanya asalie katika klabu hiyo mpaka mwaka 2026, na atakuwa akilipwa mshahara wa Pauni laki mbili na nusu ambayo ni zaidi ya milio 802 kwa pesa za kitanzania.
Stones mwenye umri wa miaka 27 mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwezi Juni mwakani 2022 lakini kwa sasa mkataba huo utaboreshwa kwa kuongezewa miaka 5. Stones alijiunga na Manchester City msimu wa 2016-17 akitokea Everton na mpaka sasa ameichezea timu hiyo michezo 168 akiwa amefunga mabao 10 kwenye michuano yote huku akiwa ameshinda mataji 8 matatu yakiwa yaigi Kuu England EPL.
4. Ni jumla ya sajili atakazo kuwa amezifanya mshambuliaji wa kimataifa wa Ubeligiji Romelu Lukaku tangu mwaka 2011 pindi atakapo kamilisha usajili wake wakujiunga na Chelsea katika dirisha hili la usajili kwa ada ya uhamisho ya pauni milion 98 ambayo ni zaidi ya bilion 311 za kitanzania na hapo jana mchezaji huyo alifanya vipimo vya afya, usajili huu utamfanya Lukaku kuwa mchezaji ghali zaidi kwenye soko la usajili ukijumuisha pesa zote zilizotumika kumnunua mchezaji huyu ambapo itafika pauni milion 291.
Usajili wa kwanza wa lukaku ulikuwa ni wa kutoka Anderlecht kwenda Chelsea Pauni milion 17, Usajili wa pili ulikuwa ni Chelsea kwenda Everton kwa Pauni Milioni 28, baada ya hapo ilikuwa ni kutoka Everton kwenda Manchester United kwa Pauni milion 75, na Manchester United kwenda Inter Mila ililipwa Pauni milion 73. Sasa inaatajwa Chelsea itailipa Inter pauni milioni 98 kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji huyo na kufanya jumla thamani yake kuwa pauni milioni 291.
Nafasi ya Pili anashika Neymar akiwa na thamani ya pauni milion 270, Cristiano Ronaldo jumla pesa iliyotumika kumnunua ni Pauni Milion 192 na Eden Hazard akiwa nafasi ya tatu kwa thamani ya pauni milion 175.
3. Ni idadi ya timu za ligi kuu zilizopata Chanjo ya Corona hapo jana katika Hospital ya taifa ya Muhimbili, timu hizo zilizopata chanjo hiyo ya uviko 19 ni Azam FC, Simba SC na Yanga Sc zote za Dar es salaam.
Timu hizo tatu zitaiwaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya vilabu barani Afrika upande wa klabu bingwa na kombe la shirikisho na timu hizo zimepata chanjo hiyo ikiwa ni sehemu ya kutimiza mahitaji ya ushiriki wa michuano hiyo mikubwa ya vilabu barani Afrika, waliopata chanjo kwenye vilabu hivyo ni wachezaji, makacho na viongozi wa vilabu hivyo na timu ya Biashara United Mara ndio timu pekee miongoni mwa zile zitakazoiwakilisha Tanznaia kwenye michuano ya kimataifa ambayo bado haijapata chanjo ya Uviko 19.
2. Ni sawa na idadi ya magolikipa waliochwa na klabu ya Yanga baada ya kumaliza mikataba yao, mabingwa hao wakihistoria wa Tanzania bara walitoa taarifa rasmi hapo jana kuwa imeachana na wachezaji wao wa nafasi ya golikipa Metacha Mnata raia wa Tanzania na Farouk Shikalo raia wa Kenya.
Wachezaji hao wanaondoka klabu hapo baada ya mikataba yao kumalizika na wote wameitumikia Yanga kwa miaka miwili. Na katika harakati za kuboresha eneo hilo Yanga imeshafanya usajili wa nyanda kutoka nchini Mali Diarra Djigui ambaye walimtambulusha Juzi na inaripitiwa wapo kwenye harakati za kukamilisha usajili wa nyanda mwingine kutoka katika klabu ya Aigle Noir ya Burundi Mtanzania Erick Johora. Lakini pia timu hiyo ya wananchi hapo jana ilimtambulisha kiungo wa kimataifa wa Uganda Khalid Aucho kuwa mchezaji wao kwa mkataba wa miaka miwili.
1. Ni nafasi iliyoshika timu ya taifa ya Olimpiki ya Marekani kwenye orodha ya mataifa yaliyochukua medali nyingi kwa ujumla ikijumuisha dhahabu, fedha na shaba, ambapo taifa hilo limechukua jumla ya medali 113, za dhahabu zikiwa 39 ambazo pia ni nyingi kuliko taifa lolote medali za fedha 41 na shaba 33.
China imemaliza nafasi ya pili ikiwa na medali 88, 38 za dhahabu 32 fedha na 18 shaba, timu ya kamati ya Olympic ya Urusi imemaliza na jumla ya medali 71 wakiwa nafasi ya 3 kwa kuchukua medali nyingi na Uingereza imebeba medali 65 na wenyeji Japan wamemaliza na Medali 58 za dhahabu zikiwa 27 wakiwa ni watatu kwa kuchukua dhahabu nyingi nyuma ya Marekani na China.



