Monday , 2nd Aug , 2021

Klabu ya Lille ambao ndiyo wanaoshikilia kombe la ligi kuu ya Ufaransa 'Ligue 1', wamefanikiwa kuendelea kuleta upinzani mbele ya matajir wa jiji la Paris, Klabu ya PSG baada ya kuwafunga 1-0 jana usiku kutwaa ubingwa wa French Super Cup kwa mara ya kwanza kihistoria nchini Ufaransa.

Timu ya Lille ikisheherekea ubingwa wa Frenc Super Cup usiku wa kuamkia leo.

Bao la pekee la ushindi lilifungwa na kiungo Miguel Xeka dakika ya 45 na kuendelea kufurahia mafanikio ya muendelezo na kujipambanu akama wapinzani wapya wa makombe kwenye ligi hiyo.

Lille imekuwa timu ya saba kubeba kombe hili nchini humo na kuwa timu ya kwanza tofauti na PSG kubeba kombe hilotokea mwaka 2012 na kusitisha utawala wa PSG wa miaka nane mfululizo.

Kombe hilo limeibua furaha kubwa kwa kocha mpya wa klabu hiyo, Jocelyn Gourvennec aliyechukua mikoba ya Christophe Galitier aliyeamua kuachia ngazi baada ya kuwapa ubingwa wa ligi kuu wa kihistoria.

PSG ilicheza bila nyota wake, Kylian Mbappe na Neymar Junior ambao wapo mapumzikoni lakini walikuwa na nyota wake wapya, Achraf Hakimi na Georginio Winjaldum pamoja na wazoefu wengine wakina Mauro Icardi, Ander Herrera na Kylor Navas ambao hawakutosha kubadili matokeo.