Friday , 30th Jul , 2021

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeweka bayana vituo vyote ambavyo vitatumika kutolea chanjo ya Corona kwa nchi nzima na katika mikoa yote.

Chanjo ya Corona

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kutokana na mwongozo wa chanjo wa Taifa dhidi ya ugonjwa huo, chanjo hizo kwa sasa zitatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa ambayo ni watumishi wa Sekta ya Afya, watu wazima wa umri wa miaka 50 na kuendelea na watu wenye magonjwa.

Tazama orodha ya hospitali zitakazokuwa zinatoa chanjo ya UVIKO-19