msanii wa Uganda Bebe Cool akiwa na gari lake aina ya Hummer
Staa huyu mkali wa nchini Uganda, kwa mujibu wa vyanzo vya karibu yake amekuwa akutumia gharama nyingi kuliweka gari hili katika oda na kufanya nalo matanuzi, na baada ya miaka miwili sasa ameamua kunyanyua mikono juu kutokana na gharama za kulimudu kuwa juu sana.
Msanii huyu katika kipindi ambacho amekuwa na gari hili ameweza kupitia matukio mbalimbali ikiwepo ajali na vilevile kuwekwa vizuizini na wanausalama kwa mara kadhaa ukiacha muda ambao ametumia kwa mafundi kwa ajili ya marekebisho.