Thursday , 1st Jul , 2021

Mchezaji nyota wa timu ya Milwaukee Bucks, Giannis Antetokounmpo na Trae Young wa Atlanta Hawks, huenda wakakosekana kwenye mchezo wa mzunguko watano wa fainali ya NBA ukanda wa Mashariki utakaochezwa alfajiri ya kuamkia kesho kutokana na majeraha.

Giannis Antetokounmpo akiwa anatolewa uwanjani baada ya kupata maumivu ya goti kwenye mchezo wanne dhidi ya Atlanta Hawks.

Giannis alipata maumivu ya goti kwenye mchezo uliopita wa mzunguko wa nne wawili hao walipokuta na Atlanta kupata ushindi wa alama 110-88 wakati alikuwa anajaribu kuzuia shambulizi na hatimaye akadondoka na kutua vibaya na kupelekea maumivu ya goti lake la kulia hiyo juzi.

Bucks walimfanyia vipimo vya MRI Giannis usiku wa kuamkia leo na majibu yakaonesha nyota huyo bado ameathirika kwenye goti na anamaumivu jambo ambalo lililopelekea kocha wake Mike Budenholzer kusema huenda nyota wake akakosekana kwenye mchezo wa mzunguko watano.

“Tutaangalia anaendeleaje kadri muda unavyozidi kwenda. Ukizungumzia uwezekano wa yeye kuwepo, nafikiri hapa lilipokifia sio pabaya lakini nikiri kuwa alianguka vibaya sana na kuathiriwa”.

Milwaukee Bucks imeshinda kwenye michezo yake miwili dhidi ya Atlanta sawa na Atlanta na kufanya michezo hiyo kuwa sare ya 2-2 hivyo kusaliwa na michezo mitatu kumsaka mshindi ambaye atapata ushindi kwenye michezo yake minne na kuwa bingwa wa ukanda wa mashariki na hatimaye kutinga fainali kuu ya NBA kuchuana na Phoenix Suns mabingwa wa Magharibi.

Hii ni mara ya pili Giannis kupata majeraha kwenye michezo ya mwisho ya mtoano ya NBA, kwani msimu uliopita alipata majeraha ya kifundo cha mguu na kuondoshwa kabisa kwenye michezo iliyosalia wakati timu yake ilipokuwa inawaongoza Miami Heat kwenye mzunguko wa pili.

Michezo hiyo ilimalizika kwa Bucks kupoteza mbele ya Miami Heat kutokana na kumkosa Giannis na Miami hatimaye akatinga fainali licha ya kwamba walifungwa na Los Angeles Lakers.

Kwa upande mwingine;

Trae Young wa Atlanta Hawks alipata majeraha kwenye mchezo wa mzunguko watatu hivyo akaukosa mchezo mmoja wa mzunguko wanne ambao timu yake iliibuka na ushindi wa alama 110-88 na kushuhudia mbadala wa Young, Lou Williams akiibuka nyota wa mchezo huo.

(Trae Young akiugulia maumivu baada ya kuumia kifundo cha mguu dhidi ya Milwaukee Bucks kwenye mchezo wa 3.)

Sio Young pekee mwenye majeraha kwa upande wa Hawks, kwani hata mlinzi wake Clint Capela aanasumbuliwa na maumivu ya jicho baada ya kupigwa kiwiko kwenye mchezo uliopita.

Taarifa kutoka Atlanta zinaeleza kuwa nyoya hao pia ni hati hati ya kutokuwepo kwenye mchezo huo.