Thursday , 1st Jul , 2021

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Wizkid anashutumiwa kuwa alimlipa mwimbaji Rihanna ili amtangazie (promote) wimbo wake “Essence” ambao alionekana akiucheza wakati ameenda live instagram.

Picha ya msanii Wizkid

Mtumiaji wa Twitter ambaye ametambulika kwa jina la Sandra Lah ameandika kuwa Wizkid na timu yake walimlipa Rihanna ili kuukuza wimbo huo kupitia mitandao ya kijamii huku akisisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa Wizkid kucheza mchezo kama huo.