Friday , 5th Dec , 2014

Wakazi wa wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuacha tabia ya kutunza fedha katika njia zisizo salama ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiharatarisha maisha yao na badala yake kuweka fedha benki ili kuwa salama.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri, wakati akizindua tawi jipya la NMB lililopo Siha mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakitaabika kwa kukosa hudumu hiyo muhimu.

Naye Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Vick Rushubo amesema benki yake imekusudia kusambaza huduma zake zaidi hasa katika kuwafikia wananchi walioko maeneo ya vijijini ambapo mpaka sasa wana matawi zaidi ya 150.

Wakiongea katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa CCM tawi la Siha Bwana Oscar Temu ambaye na Jonathani Nassari Mweyekiti wa Halmashauri wa Siha wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikosa huduma muhimu kwa wawekezaji wengi kuhofia usalama wa fedha zao.

Sambamba na uzinduzi huo misaada yenye kugharimu milioni kumi imetolewa na benki hiyo ikiwa ni pamoja na madawati yenye thamani ya shilingi million 5 kwa shule ya msingi Mwangaza na vifaa vya hospitali katika hospitali ya Kibong'oto vyenye thamani ya shilingi milioni 14