Tuesday , 15th Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bw. Bakari Msulwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bi. Sheilla Lukuba kwa kushindwa kusimamia wafanayabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametengua uteuzi huo leo, Juni 15, 2021 akiwa katika ziara yake mkoani Mwanza akihutubia vijana wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani waliowakilisha vijana wote nchini, nakusema kitendo cha kuwanyanyasa wafanyabiashara si cha kiungwana na hakikubaliki.

"Niliona juzi Morogoro vijana na wajasiriamali wadogo wamerudi maeneo yale ambayo waliondoshwa, na niliona mgambo wakienda kuwavamia kuwapiga na kuharibu vitu vyao, nimesikitika sana na lile tukio na niseme hapa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa eneo lile hawana kazi," amesema Rais Samia.

Rais Samia amehitimisha ziara yake ya siku tatu hii leo Jijini Mwanza aliyoianza tangu tarehe 13/06/2021 katika mkoa wa Mwanza.