Wednesday , 3rd Dec , 2014

Ulimwengu wa mitindo kwa upande wa Hapa Tanzania unatarajiwa kupambwa na tukio la kihistoria Ijumaa hii ambapo maonesho makubwa ya mitindo ya Swahili Fashion Week yanatarajiwa kuanza rami.

maonyesho ya mitindo na mavazi ya Swahili Fashion Week 2014

Maonesho hayo makubwa ambayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki yataendelea kwa siku tatu mfufulizo katika Hoteli ya Sea Cliff jijini Dae es Salaam.

Mbali na Maonesho ya mitindo kutoka kwa wabunifu mbalimbali, Swahili Fashion Week pia itahusisha Tuzo kwa wanaofanya vizuri katika vipengele mbalimbali vya mitindo na vilevile tamasha la manunuzi ya kazi mbalimbali za mitindo.

Wabunifu kutoka nje ya nchi watakaoshiriki katika onesho hili tayari wamekwishawasili nchini akiwepo Mbunifu Innocent Dorkenoo kutoka Ghana kati ya wengine.