
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alipotembea hospitali ya Mwanayamala Juni Mosi 2021.
Kauli hiyo ameitoa leo Juni 8, 2021, Jijini Dodoma wakati akizungumza na wanawake wa mkoa wa Dodoma na maeneo jirani ambao amezungumza nao kwa niaba ya wanawake wote wa Tanzania na kueleza kuwa kitu pekee alichokifanya kwa mwanamke huyo ni kumchua kiunoni na kumuombea na matumaini yake kwamba alijifungua salama.
"Juzi Mwananyamala nimeingia wodi ya wanaosubiri kujifungua nikamkuta mwanangu huyo anavyochachachika kujitayarisha kumleta mwanadamu ulimwenguni, nilichokifanya ni kumchua kiuno na kumpa maneno mazuri," amesema Rais Samia.
Aidha, ameongeza kuwa, "Kwa wale wazazi wenzangu nadhani mnajua wakati ule wa kusubiri kujifungua maumivu yanavyokuwa, hivyo unahitaji mtu wa kukupa maneno mazuri na kukuombea na ndicho nilichofanya kwa mwanangu yule na ni matumaini yangu alijifungua salama"