Friday , 28th May , 2021

Msanii Usher Raymond IV (Usher) na mpenzi wake Jenn wanatarajia kupata mtoto wao wa pili, taarifa hii inakuja baada ya wawili hao kuweka wazi juu ya ujauzito huo usiku wa kuamkia leo.

Picha ya pamoja Jenn na Usher

Ujio wa mtoto huyo utakuwa ni wa mtoto wa tatu kwa Usher lakini wa pili na Jenn, ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Sovereign Bo Raymond aliyezaliwa September 24, 2020.

Picha ya pamoja Jenn na Usher

Watoto wengine ni Naviyd na Usher V ambao aliwapata na aliyekuwa mkewe, Tameka Foster ambaye walioana 2007 na kutalakiana 2009.