
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Hedhi Salama Tanzania Wilhimina Malima
Bi.Wilhimina amesema hayo katika kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio ambapo amesema leo ikiwa tunaadhimisha siku ya hedhi salama inatupasa kuonyesha jinsi ambavyo tunamthamini mtu ambaye ni mwanamke katika jamii.
“suala zima la hedhi salama ni muhimu kwasababu linahitaji uweshaji wa ustawi wa binti hasa katika kutunza afya ya mwili, uzazi na utu pamoja na maendeleo ya mwanamke," amesema Bi. Wilhimina.
Pia Bi. Wilhimina ameyataja maeneo makubwa matatu ambayo yanapaswa kuangaliwa kwa umakini ili kufikia hedhi salama.
“Kuna maeneo matatu tunayaangalia katika hili, mmoja kuvunja ukimya, kutengeneza mazingira salama ya upatikanaji wa vifaa na utupaji salama, mambo haya yakisukumwa na sera, miongozo tunaweza kuwa na hedhi salama,” amesema Bi. Wilhimina.
Leo ni Maadhimisho ya Siku ya Hedhi salama ambapo kauli mbiu ni “Ukimya sasa basi, Chukua hatua na East Africa Television na East Africa Radio imezindua rasmi kampeni ya Namthamini 2021.